Next Event:
  • 00

    days

  • 00

    hours

  • 00

    minutes

  • 00

    seconds

+255 767 252 563

info@klpk.or.tz

Next Event:

  • 00

    days

  • 00

    hours

  • 00

    minutes

  • 00

    seconds

+255 767 252 563

info@klpk.or.tz

Huduma ya Uinjilisti ni huduma muhimu sana ya injili inayoliwezesha Kanisa  kutambua na kuwaunganisha watu wote waliomo katika kanisa na jinsi ambavyo neema mbali mbali za utendaji zinavyofanya kazi katika kutimiza kazi ya injili. Kwa sababu hiyo watu waliomo katika huduma ya injili wengi wao wana wito wa uinjilisti na utendaji wa wito mara nyingi hutofautiana kutoka mtu hadi mtu.

Bwana Yesu aliliagiza Kanisa kueneza injili ulimwenguni kote (Mk 16:15). Yesu alipokusudia kwenda katika miji na mahali mbali mbali, aliwatuma watu aliowachagua ili wamtangulie kwenda huko kwa kusudi la kufanya maandalizi ya safari zake za kutangaza neno la Mungu katika sehemu hizo. Aliwatuma, kati ya wale sabini aliwaweka, wawili wawili. Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe (Lk 10:1). Kwa msingi huo kazi ya injili tangu mwanzo ilipangwa na kuratibiwa ilikishirikisha wanainjili kuitenda.

Kama Yesu alihitaji watu wa kumtangulia alikokusudia kwenda, KLPK inahitaji nguvu ya pamoja zaidi. Umoja wa huduma ya uinjilisti kama Yesu alivyowatuma wawili wawili, unawapa uwezo wa kutenda kazi ya Mungu kwa nguvu zaidi, kuliko kama kazi ile ingefanywa na mtu mmoja mwenye wito wa uinjilisti.

Kwa kuwepo Huduma hii, Kanisa linapata manufaa yafuatayo:

  1. Huduma ya uinjilisti huratibu na kusimamia kazi ya injili kanisani kwa kuandaa mipango ya namna ya kutekeleza kazi hiyo na kisha kulihusisha Kanisa katika utekelezaji.
  1. Huduma ya Uinjilisti huandaa mikutano ya injili katika matawi mbalimbali ya kanisa la KLPK.
  1. Huduma ya Unjilisti hushughulika na ushuhudiaji aidha wa kundi au wa mtu mmoja mmoja.
  2. Huduma ya uinjilisti hufuatilia waongofu wapya, ambao wameokoka katika mikutano waliyofanya, ili waweze kusimama katika wokovu. Hii ni muhimu sana ili kazi iliyofanyika iweze kuzaa matunda yanayodumu.
  1. Huduma ya Unjilisti hulea na kukuza vipawa vya wainjilisti, na kuwafanya watambulike na kutumiwa na watu wengine ndani na nje ya Kanisa.
  1. Huduma ya uinjilisti inahusika na kufuatilia fedha zinazotolewa na kanisa au michango mbali mbali inayotolewa kwa ajili ya injili, na kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika sawa sawa na malengo yaliyokusudiwa.
  1. Viongozi wa huduma hii hufanya vikao mbali mbali vinavyohusu maendeleo ya injili katika kanisa. Pia wanao wajibu wa kukumbusha uongozi wa kanisa juu ya mipango mbali mbali ya injili iliyopo kanisani na jinsi ya kuifadhili ili iweze kutimizwa.

Muundo wa Huduma ya Uinjlisti katika KLPK

Muundo wa Huduma ya Uinjlisti katika KLPK unanzia ngazi ya Tawi, Parishi hadi Misheni. Mtiririko ufuatao unaonyesha muundo wa huduma hii .

Kwa kawaida shughuli za Huduma ya Uinjilisti katika Tawi huendana na mipango na utendaji wa kila siku wa Tawi, kwa upande wa Kituo Huduma hii inafanya mambo maalum yaliyopangwa na Viongozi wa Huduma ya Uinjilisti katika Parishi ili yafanywe kwa kupindi au siku husika.

Kwa ngazi ya Misheni,  Huduma ya Uinjilisti huratibu mambo yatakayofanyika Kimisheni na kushirikisha Baraza la Wazee na Wainjlisti ambapo huduma mbalimballi hufanyika ikiwa ni pamoja na Mikutano ya Injili iliyoandaliwa Kimisheni na kufanyika katika matawi.

 

Uongozi

Mwenyekiti, Mwenyekiti msaidizi, Katibu, Katibu msaidizi, Mhasibu na Mtunza Hazina. Pia Idara huwa na Mwalimu wa Kwaya ya Uinjilisti pale ambapo huduma hii ipo.